Add parallel Print Page Options

Baadhi ya Watu Wawa na Mashaka na Mamlaka ya Yesu

(Mt 12:38-42; Mk 8:12)

29 Baada ya kundi la watu kuongezeka na kumzunguka, Yesu alisema, “Ninyi watu mnaoishi sasa ni waovu. Mnaomba muujiza kama ishara kutoka kwa Mungu. Lakini hakuna muujiza utakaofanyika ili kuwathibitishia jambo lolote. Ishara pekee mtakayopata ni kile kilichompata Yona.[a] 30 Yona alikuwa ishara kwa watu walioishi katika mji wa Ninawi. Ni sawasawa na Mwana wa Adamu atakavyokuwa ishara kwa watu wa wakati huu.

31 Siku ya hukumu, ninyi watu mnaoishi sasa, mtalinganishwa na Malkia wa Kusini,[b] naye pia, atakuwa shahidi atakayeonyesha namna mlivyo waovu. Kwa nini ninasema haya? Kwa sababu alisafiri kutoka mbali, mbali sana ili ayasikilize mafundisho yenye hekima ya Suleimani. Na ninawaambia mkuu[c] kuliko Suleimani yupo hapa, lakini hamnisikilizi!

32 Siku ya hukumu, ninyi watu mnaoishi sasa mtafananishwa pia na watu wa Ninawi, nao watakuwa mashahidi watakaoonyesha makosa yenu. Ninasema hivi kwa sababu Yona alipowahubiri, walibadili mioyo na maisha yao. Na sasa mnamsikia mtu aliye mkuu kuliko Yona, Lakini hamtaki kubadilika!

Read full chapter

Footnotes

  1. 11:29 Yona Nabii katika Agano la Kale. Baada ya siku tatu akiwa katika tumbo la samaki, alitoka akiwa hai. Kisha alikwenda katika mji uliojaa uovu, mji wa Ninawi ili kuwapa watu maonyo ya Mungu.
  2. 11:31 Malkia wa Kusini Au “Malkia wa Sheba.” Alisafiri kama maili 1,000 (kilomita 1,600) ili kujifunza hekima ya Mungu kutoka kwa Sulemani. Tazama 1 Fal 10:1-13.
  3. 11:31 mkuu Kwa maana ya kawaida, “mtu mkuu zaidi”. Pia katika mstari wa 32.