Add parallel Print Page Options

Gavana Pilato Amhoji Yesu

(Mt 27:1-2,11-14; Mk 15:1-5; Yh 18:28-38)

23 Kisha kundi lote likasimama, wakampeleka Yesu kwa Pilato. Wakaanza kumshitaki Yesu na kumwambia Pilato, “Tumemkamata mtu huyu akijaribu kuwapotosha watu wetu. Anasema tusilipe kodi kwa Kaisari. Anajiita Masihi, mfalme.”

Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ni mfalme wa Wayahudi?”

Yesu akajibu, “Ndiyo, unaweza kusema hivyo.”

Pilato akawaambia wakuu wa makuhani na watu, “Sioni kosa lolote kwa mtu huyu.”

Lakini waliendelea kusema, “Mafundisho yake yanasababisha matatizo katika Uyahudi yote. Alianzia Galilaya na sasa yupo hapa!”

Pilato Ampeleka Yesu Kwa Herode

Pilato aliposikia hili, akauliza, “Mtu huyu anatoka Galilaya?” Akatambua kuwa Yesu yuko chini ya mamlaka ya Herode. Siku hizo Herode alikuwa Yerusalemu, hivyo Pilato alimpeleka Yesu kwake.

Herode alipomwona Yesu alifurahi sana. Alikuwa akisikia habari zake na kwa muda mrefu alikuwa anataka kukutana na Yesu. Herode alitaka kuona muujiza, hivyo alitegemea kwamba Yesu angefanya muujiza mmoja. Akamwuliza Yesu maswali mengi, lakini Yesu hakusema chochote. 10 Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wamesimama pale wakipaza sauti zao wakimshitaki kwa Herode. 11 Ndipo Herode na askari wake wakamcheka. Wakamfanyia mzaha kwa kumvalisha mavazi kama ambayo wafalme huvaa. Kisha Herode akamrudisha Yesu kwa Pilato. 12 Nyakati za nyuma Pilato na Herode walikuwa maadui daima. Kuanzia siku ile wakawa marafiki.

Pilato Ajaribu Kumwachia Huru Yesu

(Mt 27:15-26; Mk 15:6-15; Yh 18:39-19:16)

13 Pilato aliwaita viongozi wa makuhani, viongozi wa Kiyahudi na watu wote pamoja. 14 Akawaambia, “Mlimleta mtu huyu kwangu. Mlisema alikuwa anawapotosha watu. Lakini nimemchunguza mbele yenu nyote na sijaona hatia juu ya kitu chochote mnachomshitakia. 15 Hata Herode hakumwona kuwa ana hatia yo yote. Akamrudisha kwetu. Tazameni, hajafanya jambo lolote baya linalostahili adhabu ya kifo. 16 Kwa hiyo, baada ya kumwadhibu kidogo nitamwacha aende zake.” 17 [a]

18 Lakini wote walipaza sauti zao pamoja, “Mwue! Mwachie huru Baraba!” 19 (Baraba alifungwa gerezani kwa sababu ya kuanzisha fujo mjini na kwa mauaji.)

20 Pilato alitaka amwachie huru Yesu. Hivyo Pilato akawaambia atamwachilia. 21 Lakini walipaza sauti tena wakisema, “Mwue, Mwue msalabani!”

22 Mara ya tatu Pilato akawaambia watu, “Kwa nini? Amefanya kosa gani? Hana hatia. Sioni sababu ya kumwua. Hivyo nitamwachia huru baada ya kumwadhibu kidogo.”

23 Lakini watu waliendelea kupaza sauti. Walidai Yesu auawe msalabani. Kelele zao zikawa kubwa kiasi kwamba 24 Pilato aliamua kuwapa kile walichotaka. 25 Walitaka Baraba aliyekuwa gerezani kwa sababu ya kuanzisha fujo na mauaji aachiwe huru. Pilato akamwachia Baraba. Na kumtoa Yesu ili auawe. Hili ndilo watu walitaka.

Read full chapter

Footnotes

  1. 23:17 Nakala chache za Kiyunani zimeongeza mstari wa 17: “Kila mwaka wakati wa Siku Kuu ya Pasaka, ilimpasa Pilato kumwachia huru mfungwa mmoja.”